Kahama FM

Viongozi wa kata, vijiji someni mapato na matumizi kwa wananchi

June 18, 2024, 4:48 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Mboni Mhita {picha kutoka maktaba}

Wananchi walikataa kuhudhuria mkutano kutokana na mwenyekiti wa kijiji cha Uyogo kutokuwepo hali iliyosababisha mkutano kutokufanyika hadi leo.

Na Leokadia Andrew

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita amewataka maafisa watendaji wa kata na vijiji wa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga kufanya mikutano ya hadhara na wananchi kila baada ya miezi mitatu pamoja na kusoma mapato na matumizi ili wananchi wafahamu kilichoingia na kutoka kwenye kata yao.

Mhita ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kusiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi, ambapo amewataka viongozi wa serikali za vijiji na kata kufanya mikutano hiyo ili kuondokana na malalamiko yanayoendelea kwa wananchi.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita

Naye, mkazi wa kijiji cha Uyogo Silvester Stephano, amesema kwa hivi karibuni kumekuwa na changamoto kwa viongozi wa kata ya Uyogo kutokufanya mikutano ya hadhara na wananchi hali inayosababisha kuzorota kwa maendeleo na kumuomba mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita kulishughulia suala hilo.

sauti ya mkazi wa kijiji cha Uyogo

Akijibu hoja hizo kutokana na kutofanyika kwa mikutano kwenye kata yake, mtendaji wa kata ya Uyogo Emmanuel Msaka amesema mara ya mwisho waliitisha mkutano na wananchi walikataa kuhudhuria kutokana na mwenyekiti wa kijiji hicho kutokuwepo hali iliyosababisha mkutano kutakufanyika mpaka leo.

Sauti ya mtendaji wa kata