Kahama FM

Watoto wanaoishi mazingira magumu wawekewe mazingira wezeshi wapate elimu

June 14, 2024, 3:56 pm

kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Frola Sagasaga akiwa katika mkutano wa wadau wa elimu picha na {sebastian mnakaya }

halmashauri hiyo ilikuwa imetenga fungu ili kuwasaida watoto na baadae kilifutwa kutokana na serikali kuanzisha elimu bure

Na leokadia Andrew

Walimu wa shule za msingi na sekondari halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuwasaidia na kuwatengenezea mazingira mazuri watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kusoma na kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao.

Hayo yamesemwa  na mwenyekiti wa umoja wa walimu wa shule za msingi Msalala Daudi Mussa na mwalimu Zacharia Mganga na katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika halmashauri hiyo.

Wameiomba serikali kujenga shule maalumu kwa ajili ya watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu na kuunda mfuko maaluma wa kuwasaidia kupata elimu ili waweze kutumiza malengo hayo.

sauti ya walimu katika halmashauri ya Msalala

Naye, mtendaji wa kata ya Segese katika halmashauri hiyo Partick Mahona amesema baadhi ya wanafunzi wanamaliza kidato cha nne na wanafanya vizuri, huku wakikosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na kukosa fedha na kuomba halmashuri hiyo kuwasaidia watoto hao.

Sauti ya mtendaji wa Kata ya segese

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa halamshauri hiyo Frola Sagasaga akifafanua juu ya suala hilo amesema awali halmashauri hiyo ilikuwa imetenga fungu ili kuwasaida watoto na baadae kilifutwa kutokana na serikali kuanzisha elimu bure na kuwaomba wadau wa maendelea kupita baraza la madiwani kuona manna ya kuwasaidia.

Sauti ya kaimu mwenyekiti wa halamshauri hiyo Frola Sagasaga