Kahama FM
Kahama FM
March 29, 2026, 12:23 am

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imekabidhi vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, vikiwemo magari manne, bajaji moja na pikipiki mbili, ili kuboresha utoaji wa huduma za umeme hasa vijijini.
Na Sebastian Mnakaya
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mjini Kahama, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema hatua hiyo inalenga kusogeza huduma za umeme karibu na wananchi na kuchochea maendeleo.

Aidha, Makamba amewahimiza wananchi kuanza kutumia majiko ya umeme, hatua itakayosaidia kuhamasisha matumizi ya nishati safi, salama kwa afya, na rafiki kwa mazingira.
Salome amesema kuwa wizara ya nishati imesshelea kiasi cha shilingi milioni 85 kwa ajili ya kuimarisha na kuwa na umeme wa uhakika katika wilaya ya kahama pamoja na kuboresha miundombinu mibovu ya umeme.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Benson Mbigili, amesema vitendea kazi hivyo vitasaidia kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi.