Kahama FM

Megawati 50 za Umeme wa jua Kishapu zaikosha kamati ya Bunge

March 17, 2026, 2:26 pm

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara ya Nishati kwa kuendelea kutekeleza mkakati wa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya nishati (Energy Mix) ukiwamo mradi wa kuzalisha umeme wa jua wenye uwezo wa megawati 50 uliopo wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Subira Mgalu baada ya kamati kutembelea na kukagua mradi huo ambao tayari umeanza kuingiza umeme katika Gridi ya Taifa.

Mgalu amesema mradi huo ni kielelezo cha mapinduzi makubwa yanayoendelea kufanyika katika sekta ya nishati nchini, hususan katika jitihada za kupanua wigo wa uzalishaji wa umeme kupitia vyanzo mbadala kama nishati ya jua.

Sauti ya mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Subira Mgalu

Ameongeza kuwa hatua hiyo inaongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme nchini, hasa katika kipindi ambacho hali ya hewa imekuwa haitabiriki na kuathiri upatikanaji wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.