Kahama FM
Kahama FM
February 16, 2026, 9:25 am

”TARURA waombwa kuzitembelea barabara zilizohariba kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kuzikarabati ili zipitike na kuwaondolea wananchi adha wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza shughuli za kiuchumi”
Wakala wa barabara wa mjini na vijijini (TARURA) wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kukarabati barabara korofi na zilizoharibika kutokana na mvua zinazoendelea ili ziweze kupitika na wananchi waendelee na shughuli za kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Madiwani wa Halamshauri ya Ushetu akiwemo diwani wa kata ya Mapamba Mageta Hihumbe na diwani wa kata ya Uyogo Petro Yumbe, wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, kinachohusisha kipindi cha Oktoba hadi Desemba.
Madiwani hao wamesema kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha barabara nyingi katika halmashuri hiyo zimeharibika na kuomba TARURA kuzitembelea pamoja na kuzikarabia, huku wakianza na barabara korofi ambazo zimekuwa hazipitiki.

Akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko hayo kutoka kwa madiwani wa halmashauri hiyo, kaimu meneja wa TARURA walaya ya Kahama Mhandisi Andrea Rugina, amesema kuwa barabara zote zilizoharibika katika kipindi hiki cha mvua watazitembelea na kuzifanyia tadhimini ili zikarabatiwe.
