Kahama FM
Kahama FM
February 11, 2026, 7:44 am

”Madiwani hakikisheni miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati katika kata zenu”
Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati katika kata zao, pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu Gagi Lala, wakati wa kikao cha robo ya pili cha baraza la madiwani, ambapo amesema kuna miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa katika halmashauri hiyo, huku akiwataka madiwani kuifatilia na kuitembelea.
Aidha, Gagi amesema kuwa wamepokea taarifa mbalimbali za kamati zinazohusu miradi katika kata 20 za halmashauri hiyo, huku akimtaka mkurugezi wa Halmashauri ya Ushetu kuongeza nguvu katika miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wao, baadhi ya madiwani wa halmsahuri ya Ushetu akiwemo diwani wa kaya ya Nyamilango Charles Nkwabi na diwani wa kata ya Ulowa Gabrela Kimaro, wamesema kuwa wamepokea maelekezo hayo na watakwenda kuyatekeleza katika kata zao.