Kahama FM

Serikali yasitisha mkataba na Mkandarasi Kahama

February 8, 2026, 5:14 pm

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Masoud Kibetu akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani(Picha na Sebastian Mnakaya)

Serikali imesitisha mkataba na mkandarasi Kampuni ya Sichuan Road and Bridge Group(SRBG) aliyekuwa anatekeleza ujenzi wa miradi ya barabara za ndani katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kutokana na kutokuridhishwa na kasi yake katika kutekeleza mradi huo.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masoud Kibetu wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo cha kupokea na kujadili taarifa ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/26 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masoud Kibetu
Diwani viti maalumu Manispaa ya Kahama Herither Makaga

Awali, diwani viti maalumu Herither Makaga akiuliza swali katika kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Kahama akitaka kufahamu nini kinaendelea katika ujenzi wa barabara wa kiwango cha lami unaofadhiw na benki ya dunia kusuasu, huku akitaka kujua nini kinaendelea.

Sauti ya Diwani viti maalumu Manispaa ya Kahama Herither Makaga

Itakumbukwa Serikali iliingia mkataba na mkandarasi huyo mwezi Novemba mwaka 2023 ambapo muda wa mkataba pamoja na muda wa nyongeza umeisha bila kukamilika kwa kazi.