Kahama FM

Wananchi Kahama watakiwa kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitalo

January 22, 2026, 9:57 am

Mbunge wa jimbo la Kahama Benjamini Ngayiwa akizungumza na wananchi wa kata ya Majengo

Na Sebastian Mnakaya

Wananchi wa jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitalo ya maji pamoja na kulinda miundombinu ya barabara ili kuondokana na athari ya mafuriko ya maji wakati wa msimu wa mvua.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Benjamini Ngayiwa wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ya Kahama, ambapo amewataka wananchi kuacha kutupa kata katika mitalo hali inyosababisha uharibifu wa barabara.

Aidha, Ngayiwa amesema kuwa kwenye maeneo mengi baadhi ya miundombinu ya barabara zimeharibika baada mitalo kuziba na kusasabisha maji kuhama na kwenda kwenye makazi ya watu.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Benjamin Ngayiwa
Daraja linalounganisha kata mbili za Majengo na Nyasubi

Diwani wa kata ya Majengo, Shida Soka amesema kumekuwepo na hali ya kutochukuliwa mapema kwa takata, hali inayosababisha kutupa taka katika mitalo hiyo, huku meya wa Manispaa ya Kahama Mataluma Kaniki akiwataka wanaotupa kata kwenye mitalao waache pamoja na wanakusanya taka wakusanye kwa wakati.

Sauti ya Diwani wa kata ya Majengo, Shida Soka na meya wa Manispaa ya Kahama Mataluma Kaniki
Mbunge na diwani na viongozi mbalimbali wakikagua barabara zilizoharibika namvua

Kwa upande wake, meneja wa TARURA mkoa wa Shinyanga Avit Theodory Rugemalila amesema kuwa katika maeneo ya yaliozima mitalo na makaraviti mkandarasi wanapaswa kuyasafisha ili yasilete athari zinazosabibisha barabara kuharibika pamoja na kuwataka wananchi kuacha kutupa taka katika mitalo hiyo.

Sauti ya meneja wa TARURA mkoa wa Shinyanga Avit Theodory Rugemalila