Kahama FM
Kahama FM
October 28, 2025, 3:58 pm

”kuitunza amani tulionayo ni pamoja na kuzingatia sheria taratibu na kanuni za nchi yetu”
Na Sebastian Mnakaya
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilayani Kahama mkoani Shinyanga amewataka kuitunza amani tulionayo kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni za nchi yetu, kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika kesho oktoba 29, 2025.
Hayo yamesemwa na Makamu mwenyekiti wa wachimbaji wa madini wanawake (TAOMA) mkoa wa Shinyanga Agnes Kahabi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesma wachimbaji wako tayari kushiriki uchaguzi na kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Aidha, Agnes amesema kuwa wachimbaji wadogo wako tayari kulinda amani na utulivu tuliyonao ili kuendelea kufanyakazi na kuiletea nchi maendeleo.

Kwa upande wao, wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilayani Kahama, akiwemo Mabula Robart na Ally Matisho wamesema kuelekea uchaguzi mkuu wamejipanga kwenda kupiga kula na hawatashiriki katika maandanamo yanayohamasishwa kwenye mitandao wa kijamii.
Kila baada ya miaka mitano Tanzania huingia katika uchaguzi mkuu wa kuwachagua viongozi kwa nafasi ya Urasi, Ubunge na Udiwani, huku ikiwa imebakia siku moja kupiga kura.
