Kahama FM
Kahama FM
October 28, 2025, 3:42 pm

Wilaya ya Kahama iko salama, wananchi jitokezeni kupiga kura
Na Sebastian Mnakaya
Kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 29, 2025, Vijana wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamehimizana kushiriki uchaguzi mkuu pamoja na kulinda amani na utulivu na kuachana na maandamano.
Hayo yamesemwa leo na vijana kutoka makundi mbalimbali akiwemo madereva wasafirishaji (bodaboda), wamachinga na wachimbaji wadogo wa madini, yaliofanyika katika kiwanja vya magereza Manispaa ya kahama, mkoani Shinyanga
Aidha, vijana hao waliokusanyika katika viwanja hivyo akiwemo mwenyekiti wa bodaboda Thimoseo Gulli na mwenyekiti wa machinga Kahama Idrisa Kayombo wamesema kuwa watashiriki katika uchaguzi mkuu na kuachana na maandamao yanayohamasishwa katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda amesema wilaya ya kahama ina halmshauri tatu Ushetu, Msalala na Kahama mjiji iko salama na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura bila ya kuwa na shaka yoyote, huku akitoa tahadhari kwa ambao watakiuka sheria za nchi wakati wa kupigaji kura watachukulia hatua za kisheria.
Ikiwa imebakia siku moja uchaguzi Mkuu kufanyika wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
