Kahama FM

Miili ya wachimbaji wadogo waliofariki mgodi wa Nkandi yaagwa Kahama

February 6, 2025, 11:23 am

baadhi ya wananchi waliofika kuaga milii miwili wakiendelea na zoezi la kuaga katika hosptali ya manispaa ya Kahama

Mpaka sasa miili miwili kati ya mitatu ya wachimbaji wanaodhaniwa kufukiwa na kifusi ndani ya mgodi wa Nkandi uliopo eneo la mwime Wilayani Kahama imepatikana, huku mmoja ukiendelea kutafutwa na leo miili miwili imekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mkoani Simiyu kwa ajili ya maziko.

Na Sebastian Mnakaya

Wachimbaji wadogo wa Madini ya Dhahabu katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchukua tahadhari wakati wa shughuli za uchimbaji ili kuondokana na ajali zinazotokana na hali ya hewa iliyopo sasa.
Hayo yemesemwa jana na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita wakati wa kuaga miili ya wachimbaji wawili waliofariki dunia kutokana kufukiwa na kifusi katika mgodi wa Nkandi uliopo eneo la mwime Wilayani Kahama

Mhita amesema katika kipindi hiki cha mvua wanapaswa kuwa makini na kuchuka tahadhari katika shughuli za uchimbaji, huku akisema kuwa zoezi la uokoaji wa mwili wa tatu zinaendelea.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama

Nae Meneja wa Mgodi huo, Mdaki Shaban ameishukuru serikali kwa ushirikiano mpaka kuokoa miili miwili, huku akiomba Shirika la umeme Tanzani (TANESCO) wilaya ya Kahama kutatua changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hali inayosabisha kuwa na zoezi gumu la upatikaji na mweli wa tatu.

sauti ya meneja mgodi

Kwa upande wao, wachimbaji wa Mgodi huo, Masanja Magie amewaomba wadau wa sekta ya uchimbaji na taasisi za kiserikali kufika mapema zinapotokea majanga ya namna hiyo, huku Penina Msugua ameshukuru serikali kwa kukabidhiwa miili hiyo kwa ajili ya maziko.

sauti ya wachimbaji wadogo