Kahama FM
Kahama FM
February 3, 2025, 5:13 pm

Zoezi la uokoaji linaendelea kwa kushirikiana na wananchi, lakini linakabiliwa na changamoto ya maji mengi ndani ya duara hilo
Na leokadia Andrew
Wachimbaji watatu wa dhahabu katika mgodi wa Nkandi, eneo la Mwime, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga, wanahofiwa kufukiwa na kifusi baada ya duara walilokuwa wakichimba kumeguka katikati wakati wakiendelea na shughuli zao za uchimbaji .
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Kahama, Mkaguzi Msaidizi Hafidh Ramadhan Omary, amesema tukio hilo lilitokea february 1 2025 , majira ya saa tisa alasiri wakati wachimbaji wakiendelea na shughuli zao za uchimbaji.

Kwa upande wake, Meneja wa mgodi huo Mdaki Shaban amesema tatizo la umeme limeathiri mgodi kwa takribani wiki mbili, hali iliyosababisha maji kujaa kwenye maduara ya mgodi huo
Mmoja wa waokoaji, Joseph Marco, aliyeshuka ndani ya duara kwa lengo la kuwaokoa wachimbaji hao, amesema maji mengi yanatatiza juhudi za uokoaji ambapo amewaomba wamiliki wa migodi na wasimamizi kuhakikisha wachimbaji wanakuwa na vifaa vya kutosha kwa ajili ya usalama wao kutokana na mazingira magumu ya kazi.