Kahama FM
Kahama FM
February 1, 2025, 4:58 pm

Zaharani alikunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu manamo Januari 29 majira ya saa tano, akiwa nyumbani kwake na alipozidiwa alipelekwa katika hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa matibabu zaidi na ilipofika Januari 30 alipoteza maisha.
Na Salvatory Ntandu
Mkazi wa Kijiji cha Chambo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga Zaharani Patrombeyu (44) ambaye ni mkuu wa Shule ya Sekondari Chambo amejiua kwa kunywa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo Zaharani alikunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu Januari 29 majira ya saa tano, akiwa nyumbani kwake na alipozidiwa alipelekwa katika hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa matibabu zaidi na ilipofika Januari 30 alipoteza maisha.
Aidha Kamanda Magomi amesema Chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na amewaomba wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi huku akitoa rai kwa mtu mwenye changamoto ni vyema akawaona viongozi wa dini au wataalam wa saikolojia