Kahama FM

Wananchi watakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la zimamoto na uokoaji Kahama

January 31, 2025, 5:36 pm

Mkaguzi msaidizi wa jeshi la zima moto na uokoaji wilaya ya Kahama Hafidhi Omary{picha na Sebastian Mnakaya}

wananchi wameshauriwa kutoa taarifa mapema kwa jeshi la zimamoto na uokoaji endapo kukatokea janga la moto na majanga mengine ili liweze kutoa msaada kwa wakati

Na Sebastian Mnakaya

Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la zima moto na uokoaji ili kupunguza madhara yatokanayo na moto kwa kutoa taarifa mapema.

Wito huo umetolewa leo na Mkaguzi msaidizi wa jeshi la zima moto na uokoaji wilaya ya Kahama Hafidhi Omary, wakati akizungumza na Kahama fm, ambapo amesema kuwa utoaji wa taarifa ya mapema inapotokea majanga ya moto au ajali itasaidia kufanya ukoaji ambao hautakuwa na madhara makubwa kama ikitokea kuchelewa kutoa taarifa

Sauti ya Mkaguzi msaidizi wa jeshi la zima moto na uokoaji wilaya ya Kahama Hafidhi Omary

Katika hatua nyingine, Hafidhi amesema kuwa katika ujengaji wa nyumba zao wananchi wazingatie njia salama za upitaji wakati wa uokoaji inapotokea majanga ya moto ili kuondokana na mazingira magumu ya uokaji wa mali na watu

Sauti ya Mkaguzi msaidizi wa jeshi la zima moto na uokoaji wilaya ya Kahama Hafidhi Omary

Naye, askari wa zima moto na ukoaji wilaya ya Kahama Hoset Mmari, amemewataka wananchi kutoaingia kuzima moto ambao ni mkubwa ama kuokoa watu na badala yake watoe taarifa mapema kwa jeshi la zima moto ili lifanya ukoaji huo ambao utasaidia kuoa watu na mali na pasipo kuteta madhara makubwa

Askari wa Jeshi la zima moto na ukoaji wilaya ya Kahama Hoset Mmari{picha na Sebastian Mnakaya}

Jeshi la zima moto na ukoaji wilayani Kahama linaendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali pamoja na kufanya ukaguzi ili kuondokana na majanga ya moto yasiokuwa ya lazima.