Kahama FM

Mahakama ya wilaya Kahama yazindua wiki ya sheria

January 27, 2025, 11:52 am

Jengo la mahakama ya wilaya ya Kahama

kauli mbiu ya mwaka huu ‘‘Tanzania ya 2025 nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo mkuu ya dira ya Taifa ya maendeleo’’

Na Sebastian Mnakaya

Wananchi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mahakama ya wilaya ili waweze kupatiwa elimu ya Sheria kutoka kwa taasisi mbalimbali za serikali katika wiki ya sheria iliyozinduliwa

nchini.

Wito huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Kahama Edmund Kente, katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya sheria katika manispaa ya Kahama, ambapo amesema kupitia wiki hiyo, watatoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya sheria katika viwanja vya Mahakama.

Aidha, Kente amesema wataendelea kutoa elimu sehemu mbalimbali katika manispaa ya Kahama kwa makundi, ikiwemo shuleni, stendi na kwenye mkusanyiko wa watu ili kila mwananchi anufaike na elimu hiyo ya sheria inayotolewa bure kwa wiki nzima.

sauti ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Kahama Edmund Kente,

Nae, wakili wa kijitegemea ambaye pia ni mwanachama wa chama cha mawakili Tanzani (TLS) Martine Masanja amesema watashirikiana na Mahakama katika kutoa elimu kwa wananchi, huku Neema Manase mdau wa sheria ameishukuru serikali kwa kushirikiana wadau kuwapatia elimu wananchi waijue sheria mbalimbali za nchi.

sauti ya wadau wa sheria

Mahakama ya wilaya ya Kahama imezindua wiki ya sheria na  Kilele chake inatarajiwa kufanyika hadi februari 3 mwaka huu, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ‘‘Tanzania ya 2025 nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo mkuu ya dira ya Taifa ya maendeleo’’