Kahama FM

Wananchi fanyeni makubaliano ya kimkataba

January 17, 2025, 2:06 pm

Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Kahama Edmund Kente, akizungumza na Kahama fm ofisini kwake [picha na Sebastian Mnakaya]

Maonesho ya Wiki ya sheria yataanza January 27 mwaka huu, hadi siku January 31 mwaka huu katika viwanja vya mahakama ya wilaya Kahama

Na Sebastian Mnakaya

Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa na tabia ya kufanya makubaliano ya kimkataba wakati wa kukopeshana fedha pamoja na kuuziana vitu mbalimbali ili wanaposhindwana na linapokuja kwenye vyombo vya sheria liweze kushughulikiwa.

Agizo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Kahama Edmund Kente, wakati akizungumza na Kahama fm ofisini kwake ambapo amesema kuwa wananchi hawapaswi kufanya mambo kienyeji na badala yake wafanye kisheria ili inapotekea changamoto liweze kutatuliwa kisheria.

Aidha, Kente amesema katika eneo ambalo wananchi wengi wanapata changamoto ni aina ya mikataba ambayo wanawekeana na mengine inawasababisha kupoteza vitu vya dhamani, huku akiwataka kuwa makini katika ujazaji wa mikataba hiyo.

sauti ya Edmund Kente,

Kwa upande wake, kaimu mwenyekiti wa shirikia la kutetea haki za kibinadamu (SHIHABI) wilayani Kahama Solomi Butigwa, amesema kuna baadhi ya watu wanaokopesha wamekuwa sio waamini hali inayosababisha kuwadhurumu mali zao kwa kuwapatia mikataba mibovu.

Sauti ya kaimu mwenyekiti

Naye, mwanasheria wa shirikia la kutetea haki za kibinadamu (SHIHABI) AliphoceMagongo amewataka wananchi kuwa na utamaduni kuingia mikataba kwa maandishi ili kuondokana na hali ya kudhurumi mali ama fedha zao waendapo mahakamani pamoja na kuwashirikisha wana sheria.

Sauti ya mwanasheria

Mahakama ya wilaya ya Kahama inatarajia kuanza wiki ya sheria January 25 mwaka, huku Kilele chake ni febuar 3, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ‘‘Tanzania ya 2025 nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo mkuu ya dira ya Taifa ya maendeleo’’