Mwenge wa Uhuru wazindua Jengo jipya la uchunguzi Kahama
August 15, 2024, 10:45 pm
watumishi wa sekta za afya endeleeni kutoa huduma nzuri kwa wananchi baada ya serikali kutengeneza miundombinu rafiki kufanyia kazi
Na Kitila Peter
Halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imepongezwa kwa kuendelea kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo, afya, barabara na shule.
Hayo yamesemwa leo na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava, wakati kifungua mradi wa jengo la uchunguzi la kisasa katika manispaa ya kahama, ambapo amewataka watumishi wa sekta za afya kuendelea huduma nzuri kwa wananchi baada ya serikali kutengeneza miundombinu rafiki kufanyia kazi
Kwa upande wake mganga wa hospitali ya manispaa ya Kahama Fredrick Malunde, wakati akisoma taarifa mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge amesema kuwa mradi huo wa jengo la uchunguzi la kisasa limegharimu kiasi cha zaidi shilingi billion 1.9 mpaka ukamilika kwake.
Awali, mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imendelea kutoa fedha nyingi katika sekta mbalimbali ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo kwa kupata huduma zilizobora pamoja na kutotembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.