Ripoti za (CAG) kwa Asasi za Kiraia umetajwa kuchangia kasi ya ufuatiliaji wa Miradi
July 15, 2024, 3:53 pm
Na Sebastian Mnakaya
Uwasilishwaji wa Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kwa Asasi za Kiraia mkoani Shinyanga umetajwa kuchangia kasi ya ufuatiliaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye jamii ikilinganishwa na hapo awali.
Ni katika Mafunzo ya Asasi za Kiraia 25 mkoani humo na Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG cha dhima ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuchambua taarifa za ukaguzi kupitia toleo la Maalumu la Mwananchi, ambapo Musa Ngangala na Cecilia Msangwa ni Viongozi wa Asasi za Kiraia wamesema ofisi ya CAG kutoa taarifa mapema ili wao waweze kuandika maandiko wenye tija katika asasi zao.
Nae, Focus Mauki Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kutoka Ofisi ya CAG ametaja dhima ya mafunzo hayo huku Kaimu Mkaguzi wa mkuu wa hesabu za nje mkoa wa Shinyanga akitaja faida za uwasilishwaji wa taarifa za CAG kwa Wananchi.