Wanahabari Shinyanga watembelea kituo cha uzalishaji maji Ziwa Victoria, Ihelele
May 7, 2024, 1:03 pm
Kituo cha uzalishaji maji Ziwa Victoria uliopo Ihelele wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza picha na (Sebastian Mnakaya)
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wametembelea Kituo cha uzalishaji ya Ziwa Victoria Kilichopo Ihelele wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, Maji ambayo huzalishwa kupitia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KASHWASA).
Na Sebastian Mnakaya
Mradi wa Kituo cha uzalishaji maji ziwa Victoria cha Ihelele, wilayani Miswingi mkoani Mwanza kinauwezo wa kuzalisha lita milioni 80 kwa siku na kwa sasa kinazalisha lita milioni 67 kutokana na uhitaji wa watumiaji maji katika mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani
Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Kahama (KASHWASA) JOHN ZENGO, wakati wa zira ya mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa huo, yalioandaliwa na EWURA kanda ya magharibi, ambapo amesema mradi huo mpaka sasa unahudumia mikoa sita
Nae, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji( EWURA) kanda ya Magharibi Eng. WALTER CHRISTOPHER, amesema kuwa kazi kubwa wanayoifanya ni kuangalia uzalishaji wa maji hayo, yako kwenye ubora pamoja na kujua gharama halisi ili kuweka bei rafiki kwa mzalishaji na mtumiaji.
Kwa upande wao makamu mwenyekiti wa shinyanga press club (SPC) PATRICK MABULA na JOSEPH MBATALA mjumbe wa kamati ya watumia wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA wameishuru EWURA kwa kuwapatia mafunzo hayo kwa vitendo ambapo watakwenda kuwaelimisha jamii pamoja na kuwaeleza sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko yao