Kahama FM

Wakazi Kata ya Nyandekwa wahimizwa ushirikiano ujenzi wa zahanati

July 4, 2023, 11:20 am

kahama
Mmoja wa wananchi wa Kata ya Nyandekwa Wilaya ya Kahama akizungumza kwenye mkutano na Diwani wa Kata hiyo juu ya ujenzi wa zahanati: Picha na Steve Mathias

Wakazi wa Bujika kata ya Nyandekwa wilayani Kahama wametakiwa kuacha kukwamisha  shughuli  ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo.

Na Clement Paschal

Wakazi wa kijiji cha Bujika kata ya Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha kukwamisha  shughuli  ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo na badala yake washirikiane kuhakikisha wanafanikisha ujenzi huo.

Kijiji cha Bujika kimepatiwa kiasi cha million 50 kuhakikisha kina kamilisha ujenzi wa zahanati

Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya Nyandekwa Menard James wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, ambapo amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya wananchi kukwepa kutoa michango ya ujenzi wa zahanati hiyo licha ya uongozi wa kata hiyo kufanya juhudi mbalimbali kuhakikisha ujenzi huo unakamilika.

Aidha Menard ameongeza kuwa hadi hivi sasa kuna miradi mbalimbali ambayo tayari imewekewa fungu la utekelezwaji wake, ikiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya Nyandekwa kiasi cha million 50.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Nyandekwa wilaya ya Kahama, Menard James akitoa wito kwa wananchi wa kata yake kutoa ushirikiano katika ujenzi wa zahanati

Akizungumza kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Kahama katibu wa mbunge Abdual Mpei amesema kuwa kijiji cha Bujika kimepatiwa kiasi cha million 50 kuhakikisha kina kamilisha ujenzi wa zahanati hiyo ili kuepukana na adha ambazo wakaazi wa kijiji hicho walikuwa wakizipata kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya katika vijiji jirani.