Upungufu wa chakula: Wananchi watakiwa kuhifadhi mazao ya chakula
July 3, 2023, 12:17 pm
Wananchi wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameaswa kuhifadhi mazao katika msimu huu ili kuepuka uhaba wa chakula.
Na Sebastian Mnakaya
Wananchi wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuhifadhi mazao ya chakula kutokana na upungufu uliopo kwa msimu huu, pamoja na kusubiri bei kupanda kwa baadhi ya mazao ili yaweze kuwasaidia katika kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo
Rai hiyo imetolewa na afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya Ushetu Mogani Mwita, ambapo amesema kuwa katika kipindi hiki cha uvunaji wakulima wanapaswa kuwa waangalifu kwa kutouza chakula chote kwa ajili ya kaya zao badala yake watunze pamoja na kusubiri bei.
Mogan ameongeza kuwa katika mazao ya biashara wakulima wametakiwa kutouza mazao yao shambani kabla ya kuvunwa na wanapouza wanapaswa kutunza fedha hizo ili waweze kupata bei nzuri pamoja na kuwashirikisha wenza wao ili kuondokana na migogoro ya kifamilia.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyamilangano Robert Mihayo amesema kuwa wakulima wa mazao mbalimbali, kwa msimu wanapaswa kutunza chakula kutokana na chakula kuwa sio kingi na kuwaomba wakitunze kwa ajili ya kuwanufaisha kwa siku za baadaye.
Aidha amemuomba Kamishna wa Polisi wa Oparesheni na Mafunzo nchini Awadh Juma kufikisha ombi la Kagera kuwa kanda maalum kutokana na mauaji yanayotokea kila siku ambapo ni wastani wa mtu mmoja na kwa mwezi watu 28 hadi 30.