DR KITIMA:Wanaume na wanawake wote wana haki ya Kuishi,Acheni mauaji.
February 14, 2022, 3:31 pm
DAR ES SALAAM
Jamii imetakiwa kuelewa kuwa wanaume na wanawake wote wana haki sawa ya kuishi na kufanya shughuli zozote zilizo halali na kwamba wanaume waache tabia ya unyanyasaji na mauaji yanayofanywa dhidi ya wanawake.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki hii na Katibu mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC) Dr Charles Kitima katika mdahalo uliofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu haki za wanawake na mauaji ya Kikatili nchini Tanzania.
Katika hatua nyingine Dr Kitima Ameongeza kuwa nchini Tanzania kwasasa mauji ya wanawake yanaondelea ni dhana potofu kuwa mwanamke ni chombo cha mwanaume na kwamba jamii imesahau kuweka haki za binadamu katika mila na desturi.
Naye Mwakilishi kutoka ofisi ya Mufti mkuu wa baraza la waislamu Tanzia Sheikh Swed Twaibu Swed ametoa wito kwa vyombo vya dola na mabaraza ya usuluhishi kumaliza kesi kwa wakati hasa za Mirathi ili kuondoa hali ya wanawake kuchanganyikiwa na kufanya maamuzi yasiyo sahihi.
Kwa upande wake Kamishina wa Tume ya haki za binadamu na Utawala bora Tanzania Dr Fatma Khalfan ameitaka jamii kujitokeza kupaza sauti inapoana unyanyasaji na kuacha tabia ya kukaa kimya na kusema hayo ni mambo binafsi.
Mdahalo huo uliofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu haki za wanawake na mauaji ya Kikatili nchini Tanzania umeratibiwa na Shirika la Freedom House na Kuhudhuliwa na watu zaidi ya mia moja.