LEAT
Kahama FM

GEITA: LEAT yawapiga msasa madiwani 52 kuhusu sheria za madini na Utunzaji Mazingira.

November 22, 2021, 5:56 pm

Diwani wa Kata ya Kamena Peter Kulwa akiongea kwenye Semina Hiyo.

GEITA

Madiwani wa halmshauri ya mji Geita Mkoani Geita wameiomba serikali na wadau wa maendeleo kuwapa elimu ya sheria ya ardhi na madini mara kwa mara ili kuwasaidia kuwa na uelewa kuhusu  haki zao za msingi.

Madiwani wametoa Wito huo  leo mkaoni Geita katika semina ya sheria ya uziduaji ya kuwajengea uwezo wa  kuzitambua sheria za madini na ardhi katika maeneo yao wanayozunguka.

Sauti za Madiwani wakiomba Semina zitolewe mara kwa mara.

Nao baadhi ya madiwani wa viti Maalumu halmashauri ya mji wa Geita Winifrida Malunde na Evelina Mlyabuso wameiomba serikali kuwapa kipaumbele wanawake katika sekta ya uziduaji ikiwemo kuwapatia mikopo mikubwa  ili iwasaidie katika uchimbaji wa madini.

Madiwani wa Viti maalamu wakiongelea Ushirikishwaji wa wanawake katika Sekta ya Uziduaji.

Naye mwezeshaji wa semina hiyo kutoka timu ya wanasheria watetezi wa Mazingira (LEAT) wakili Baraka Thomas amesema kuwa semina hiyo imelenga kuwafundisha madiwani kuhusu utambuzi wa sheria za uziduaji na umiliki wa ardhi.

Sauti ya Wakili kutoka Timu ya wanasheria watetezi wa Mazingira (LEAT) Baraka Thomas
Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakiwa katika Semina hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Busanda Tumaini Magesa amewashukuru Timu ya wanasheria watetezi wa Mazingira (LEAT) kwa kutoa semin hiyo kwani zitawafungua madiwani katika kujua sheria nyingi za ardhi na madini.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Busanda Tumaini Magesa

Semina hiyo ya mafunzo ya siku mbili iliyoanza Leo mkoani Geita imeandaliwa na timu ya wanasheria waetetezi wa Mazingira (LEAT) imejumuisha jumla ya madiwani 38 wa kata za halmashauri ya mji wa Geita na madiwani 13 waviti maalumu.