Kahama FM

KAHAMA: Zaidi ya Wakulima 320 wamegawiwa mbegu bure za zao la pamba

November 4, 2021, 4:13 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akigawa mbegu kwa wakulima wa pamba

Zaidi ya Wakulima 320 wa zao la pamba katika kata ya Nyakende Halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani Shinyanga wamepatiwa mbengu bure za zao la pamba zilizotolewa na serikali katika kuwainua wakulima hao katika zao hilo la kibiashara.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa mbegu hizo katika kata ya Nyakende, mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA, amesema kuwa wametoa mbegu hizo bure kwa kila kijana mwenye umri wa miaka 14 ambaye sio mwananfunzi kulima heka nne na atakayeshindwa kulima atachukuliwa hatua.

Kwa upande wake afisa kilimo wa kata ya Nyakende katika Halmashuri hiyo VIDISINT MAMLIMA, amesema kuwa wakulima waliopatiwa mbegi hizo wanapaswa kulima kitaalum ili waweze kupata pamba nzuri kwa ajili ya kupata soko zuri katika kipindi cha ununuzi.

Nao, wakulima wa zao la pamba katika kata ya Nyakende wakizungumza na kahama fm kwa nyakati tofauti wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais SAMIA SURUHU HASSAN kwa kuwapatia mbegu za pamba bure, ambapo zimewapunguzia gharama za kununua mbegu hizo.

Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya KAHAMA FESTO KISWAGA amewataka wakulima katika wilaya yake kulima mazao ya biashara pamoja na tumbaku, pamba na choroko ili kijikwamua kiuchumi.