kahama
Kahama FM

KAHAMA:Tamasha la Michezo,Afya na biashara kuanza leo,Wafanyabiashara 3000 kushiriki.

August 23, 2021, 7:47 am

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga

Zaidi ya wafanyabiashara 3000 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania wanatarajia kushiriki mazoezi ya viungo ili kujikinga na ugonjwa wa Uviko 19 pamoja na Maonesho ya Biashara yatakayofanyika katika uwanja wa taifa wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuanzia Jumatatu Agosti 23 hadi Agosti 29,2021.

Kauli hiyo imetolewa leo  Jana Agosti 22,2021 na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Michezo, Afya na Biashara litakalohusisha mazoezi sambamba na maonesho ya biashara likalofanyika wilayani humo kuanziaAgosti 23 hadi 29 mwaka huu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.

Amesema serikali kwa kushirikiana na Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama wameaandaa mazoezi hayo ya siku saba yatakayokwenda sambamba na maonesho ya biashara ili kutoa fursa kwa wananchi wa Kahama kutangaza bidhaa wanazozizalisha.

Kiswaga amefafanua kuwa mazoezi hayo yanalenga kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani katika mapambano dhidi ya gonjwa la Corona kwa kuwahimiza wananchi kutenga muda wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Festo Kiswaga

Sambamba na hilo Kiswaga amewahakikishia usalama wafanyabiashara wote watakaoshiriki mazoezi na maonesho hayo ya biashara kwa siku hizo saba.

Kwa upande wake, Mratibu wa Tamasha la Michezo, Afya na Biashara kutoka Taasisi ya GS1 Tanzania Shabani Mikongoti amesema kuwa maandalizi yote ya mazoezi na maonesho hayo yamekamilika na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kushiriki maonesho hayo maalumu.