Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
January 5, 2026, 6:39 pm

Ni mafunzo ya mfumo wa School Information System.
Na Devi Moses
JUMLA ya walimu 110 kutoka Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wameshiriki mafunzo ya matumizi ya mfumo wa School Information System (SIS) yaliyofanyika ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa Day.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo walimu katika ukusanyaji, uhifadhi na usimamizi wa takwimu za shule kwa kutumia mfumo wa kidijitali.
Akizungumza kuhusu faida za mfumo huo, mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ichenjezya Lukasi Mwambela amesema
Kwa upande wake, mtaalamu wa TEHAMA kutoka Shule ya Msingi Ihanda, Joshua Kibona, ameahidi kwenda kuwafundisha walimu wenzake ili kuhakikisha usahihi wa ukusanyaji takwimu.
Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Vwawa, Pelesi Mwakalinga, amefafanua kuwa mfumo wa SIS utakuwa msaada mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya elimu.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wilaya ya Mbozi amesema mafunzo haya ni endelevu kwa walimu wa aina hiyo shule zote