Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
September 21, 2025, 8:56 pm

Umoja wa Machifu umefanya dua maalumu kusisitiza amani, utulivu na mshikamano
Na Devi Mgale
UMOJA wa Machifu Mkoa wa Songwe umefanya dua maalumu ya kuombea uchaguzi wa mwaka huu uwe wa amani na utulivu.
Dua hiyo imefanyika Septemba 20, katika Kata ya Mpemba, Wilaya ya Momba, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo, Chifu Mlotwa Msangawale, pamoja na Katibu wake, Maringa Mkoma. Katika kikao hicho maalumu, wajumbe wameshiriki kwa dua mbalimbali.
Chifu Msangawale ameombea majeshi yawe imara na kuwataka machifu wengine warudi kundini.
Aidha, Katibu wa Umoja huo, Maringa Mkoma, amewakumbusha wajumbe wajibu na majukumu waliyopewa na Chifu Hangaya, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.