Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
September 11, 2025, 4:47 pm

Ni ya utoro, wizi na uharibifu
Na Asteria Kibiki
Watoto wanaojihusisha na vitendo vya kuokota vyuma chakavu katika kata ya Ichenjezya, wilayani Mbozi mkoani Songwe wanatuhumiwa kuongoza kwa utoro shuleni na kujifunza tabia za wizi na uharibifu.
Pamoja na kutoroka shuleni , watoto hao wanadaiwa pia wanajifunza tabia mbaya zikiwamo za wizi wa masufuria na kukata vyuma vya Serikali vikiwamo vibao vinavyoonesha majina ya vitongoji na mitaa.
Ofisa Mtendaji wa Kitongoji cha Ichenjezya, Agness Shitindi, amesema hayo alipozungumza na Vwawa Fm iliyotaka kujua sababu za vibao vingi kuharibiwa katika kitongoji hicho.
Baadhi ya wazazi katika kata ya Ichenjezya wamekiri kuzumbe katika malezi huku wakitoa wito kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wao ili kuzuia vitendo vya watoto kukatisha masomo na kuzurula mtaani.