Uyui FM
Uyui FM
3 October 2025, 9:05 am

Na Zabron G Balimponya
Wahudumu wa kutoa huduma ya nyama katika mabucha wameshauliwa kutouza kipande cha nyama chenye muhuri wa daktali hadi kiwe cha mwisho ili kipande hicho kitumike kumlidhisha mteja kwamba nyama hiyo imepimwa na ni salama kiafya
Hayo yameelezwa na Msimamizi wa bodi ya nyama kanda ya magharibi Abdallah Waziri wakati akifanya mahojiano na UFR ambapo pia amewasihi wahudumu hao kupima afya zao ili kuepukana na magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kifua kikuu

Baadhi ya Wakazi wa Manispaa ya Tabora wametoa maoni yao juu ya uelewa wa namna gani wanaweza kuhakikisha usalama wa nyama wanapokwenda buchani kununua
Kwa mujibu waMsimamizi wa bodi ya nyama kanda ya magharibi Abdallah Waziri kila mnunuzi wa nyama katika bucha anayo haki yake ya msingi kuomba cheti kinacho onyesha taarifa za muhudumu wa bucha kama cheti hicho ni salama na kinaonyesha hali salama ya afya ya muhudumu huyo