Uyui FM
Uyui FM
2 October 2025, 7:58 pm

Serikali yaombwa kutoa ushirikiano kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Na Zabron G Balimponya
Serikali imeombwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha wa kutambua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuwatambua wale wanaoweza kuwasaidia kutoka katika hatali hiyo ili watoto hao waweze kutimiza malengo yao ikiwemo elimu
Ombi hilo limetolewa na Eva Eliafoo ambae ni mwentekiti wa shirika la Camfed mkoa wa Tabora September 27, 2025 kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Mirambo wakati akisoma lisara ya mafanikio na changamoto zilizopo kwenye shirika hilo katika kusaidia watoto walopo katika mazingira hatarishi.
Raphaeli Mageni ni Afisa elimu kata ya Mwinyi alie muwakilisha Afisa elimu wilaya manispaa Tabora ameahidi kuwa atatoa ushirikiano na changamoto hizo ziweze kutatuliwa.

Kwa upande wake mratibu wa miradi ya Shirika la Camfed Manispaa Tabora Levina Pius amesema kwa sasa wanaendelea na mpango wa kufikia wilaya zote za mkoa ili kuwafikia watoto waliopo mazingira hatarishi na kuwasaidia
Felsta Michael ni Katibu wa Camfed mkoa wa Tabora ameelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2025
Kwa mujibu wamratibu wa miradi ya Shirika la Camfed manispaa Tabora Levina Pius Tanzania ni miongoni mwa nchi 6 barani Africa zinazo nufaika na shirika hilo huku Tanzania ikitekeleza miradi yake kwa mikoa 10 ikiwemo Tabora