Uyui FM
Uyui FM
27 September 2025, 7:14 pm
“Serikali inaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa sambamba na kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji”, Paul Chacha.
Na Wilson Makalla
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amewataka wafanya biashara ndogondogo Mkoani Tabora kujiweka kwenye vikundi na kutumia fursa za kidijitali kwa kuomba tenda kwa wazabuni kwa kutumia mfumo wa manunuzi wa serikali (NeSt) ili kujikwamua kiuchumi kupitia mfumo huo.
Chacha ameyasema hayo Septemba 24, 2025 akiwa mgeni rasmi katika kongamano la wafanyabiashara ndogondogo kutoka wilaya za mkoani humo lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, maarufu Chuo cha Uhazili kilichopo nadani ya Manispaa ya Tabora.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali waliohudhuria kongamano hilo wamesema wamepata ujuzi na maarifa muhimu yatakayowezesha biashara zao kukua huku wakiahidi kujiunga na mfumo wa manunuzi ya serikali na kuomba tenda.

Kongamano hilo lililenga hasa kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao pamoja na kuwajengea uelewa wa kukua kibiashara kwa kuzikimbilia fursa mbalimbali.