Uyui FM

Kiswahili kuongeza uelewa wa kisheria mahakamani

27 September 2025, 6:30 pm

Na Wilson Makalla

Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuendesha kesi yameendelea kuibua maoni mkoani Tabora ambapo wanasheria na wananchi wametoa maoni kuhusu nafasi ya Kiswahili kwenye mfumo wa kimahakama.

Wakili wa Kujitegemea kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Akram Magoti amesema Kiswahili kina nafasi kubwa ya kuongeza uelewa kwa wananchi kwa kuwa ni lugha ya Taifa ingawa bado kunaa changamoto ya ukosefu wa istilahi rasmi za kisheria zilizotafsiriwa kwa Kiswahili.

Wakili Akram Magoti katika mahojiano na UFR
Sauti ya Wakili Ikram Magoti

Kwa upande wao wananchi wa manispaa ya Tabora wamesema mara nyingi lugha ya kingereza inafanya washidwe kuelewa hivyo wameshauri kesi ziendeshwe kwa lugha ya Kiswahili ili kuwepo na uelewa.

Maoni ya baadhi ya wakazi wa Tabora

Magoti amesisitiza wananchi kuwa na utaratibu wa kuuliza mambo yanayohusu sheria kwa wanasheria ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza.