Tadio yatoa mafunzo kwa radio za kijamii Zanzibar
10 August 2023, 8:47 am
Kuchapisha tarifa katika mtandao wa radio TADIO kutaongeza idadi ya wafuatiliaji wa tarifa za radio za kijamii.
Na Vuai Juma.
Wandishi wa habari wa radio za kijamii Zanzibar wametakiwa kuitumia fursa ya kutuma kazi zao katika mtandao wa radio tadio ili ziweze kuwafikia watu wengi kote ulimwenguni.
Hayo yamesemwa na mhariri wa mtandao huo Hilali Ruhundwa mara baada ya kufunga mafunzo ya siku mbili kwa radio za kijamii zilizo chini Tadio kwa kanda ya Zanzibar yaliyokuwa na lengo la kuwaelimisha namna ya kuchapisha habari kwenye mitandao yaliyofanyika ukumbi wa mikutano ZSSF Kariakoo Zanzibar.
Amesema kwa sasa mambo ya uandishi wa habari yamekuwa yanabadilika kila wakati hivyo ni lazima wanahabari wawe wanapatiwa elimu ili waweze kuendana na mabadiliko hayo.
Naye Katibu Mtendaji wa TADIO ndugu Ali Khamis amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa vyombo vya habari hasa vya kijamii lakini bado baadhi yao vimekuwa vikishindwa kutuma kazi zao kwenye mtandao kutokana na kukosa gharama za bando pamoja na utafutaji wa habari huku akivitaka vyombo hivyo kujitahidi kulingana na uwezo wao.