Wakulima wa mwani Tumbatu watakiwa kuacha mazoea katika kazi zao
30 September 2023, 8:27 am
Zao loa mwani ni kilimo muhimu ambacho kinafaida katika maisha ya binadamu hivyo ni wajibu kukiendeleza. Na Makame Pandu.
Wakulima wa mwani kisiwani Tumbatu wametakiwa kufanya juhudi zitakazowawezezesha kulima zao hilo kwa wingi zaidi ili waweze kujikwamua na umaskini.
Akifungua mafuzo ya kuwajengea uwezo wakulima hao yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la afisi ya wilaya hiyo Katibu Tawala wilaya Ndogo Tumbatu Khatibu Habibu Ali amesema Kwasasa zao la mwani limekua ni muhimu kwani limekuwa likikuza uchumi wananchi.
Amesema ipo haja ya kukifanya kilimo hicho kuwa cha kisasa zaidi ili waweze kufaidika na fursa zitokanazo na zao hilo.
Aidha amewataka kuyafanyia kazi mafuzo wanayopewa kwani kufanya hivyo kutawapelekea kuwa wabunifu na kuwaongezea ufanisi katika shughuli zao.
Nae afisa utafiti kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu Ndugu Yusuf Bakari Salim amesema lengo la mafuzo hayo ni kuwajengea uwezo wakulima hao ili wawe na uwezo wa kulima kilimo chenye tija na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa mafunzo hayo ili waweze kutoa faida kwa wengine.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamewameishukuru wizara ya uchumi wa buluu pamoja na ldara ya Maendeleo ya Ushirika kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili waondokane na kilimo cha mazoea.
Mafuzo hayo ya siku mbili yamefadhiliwa na Good Neighbors Tanzania nayamewashirikisha wakulima 35 wa kisiwa cha Tumbatu.