Savvy FM
Savvy FM
February 24, 2026, 9:40 am

Uzinduzi huo umefanyika wakati wa kampeni ya NG’ARISHA JIJI inayolenga kuhamasisha usafi wa mazingira na kujenga utamaduni wa utunzaji wa Mji.
Na Mariam Mallya
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, hivi karibuni amezindua rasmi vikundi vya vijana vya ukamataji wa wachafuzi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usimamizi wa usafi wa Mazingira katika Jiji la Arusha.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Kata ya Kaloleni na Ngarenaro, Dc Mkude amesisitiza kuwa vikundi hivyo vitakuwa na jukumu la kuwabaini, kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika kuchafua mazingira, ikiwemo kutozwa faini ya shilingi 50,000 kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranghe amesema vikundi hivyo vitawapiga faini wananchi na wafanyabiashara wote wanaochafua mazingira na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na nidhamu na kuepukana na rushwa.