

February 18, 2025, 6:26 pm
Tukio limetokea Febuari 15 katika kijiji hicho na kuhusisha watoto wanne wa kike wa familia mbili tofauti ambao walikuwa wakiogelea katika bwawa hilo
Na Salvatory Ntandu
Wakazi watano wa Kijiji cha Bulige Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefariki dunia kwa kuzama kwenye maji ya Bwawa lililochimbwa na wakandarasi wa ujenzi wa barabara ambalo limetajwa kuhatarisha usalama wa wakazi wa eneo hilo.
Tukio hilo limetokea Febuari 15 katika kijiji hicho na kuhusisha watoto wanne wa kike wa familia mbili tofauti ambao walikuwa wakiogelea katika bwawa hilo ndipo mama wa watoto wawili kati ya wanne waliopteza maisha alipobaini uwepo wa tukio hilo alikwenda kuwaokoa nae akazama na kufariki dunia.
Nae, Mwenyekiti wa Kiijiji cha Bulige, Allen Mahanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja Waliopoteza Maisha ni Pamoja na Hoja Kubo (29) Rachel Peter (11) Samike Peter (1) Wengine ni Zawadi Nkwabi (13)Khadija Nkwabi 11 ambao walikuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Bulige.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Wilaya ya ya Kahama, SSP Stanley Luoga ametaja hatua zilizochukuliwa, huku Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akitoa kauli ya Serikali kwa wakandarasi wanaotekeleza ujenzi.