Kahama FM

KAHAMA:Serikali ya manispaa ya kahama imezindua mwongozo wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU

December 16, 2021, 12:32 pm

Serikali ya manispaa ya Kahama imezindua mwongozo wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kwa vijana wa skauti ili kuwawezesha kupambana na rushwa katika maeneo yao……

Katibu tawala wa manispaa ya Kahama TIMOTHY NDANYA ambae amezindua mpango huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA, amesema serikali imeamua kuweka mpango huo ili kufundisha maadili na uzalendo kwa vijana ili wawe sehemu ya kusambaza elimu hiyo…….

NDANYA amewataka wanafunzi kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini kwa kuwa uzalendo kwa nchi ni mhimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa……

Amesema rushwa inaweza kutokomezwa ikiwa watu watakuwa wazalendo na kupata mafunzo wakiwa bado ni wadogo…..

Kwa upande wake mkuu wa taasisi ya kuzuia a kupambana na rushwa TAKUKURU manispaa ya Kahama ABDALLAH URARI amewataka vijana wa skauti kusambaza elimu ya kupambana na rushwa waliyoipata……

Kamishina wa skauti manispaa ya Kahama, ambae pia ni mkufunzi msaidizi wa skauti mkoa wa shinyanga amesema mpango huo utazifikia shule za sekondari na shule za msingi.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo ya skauti na mpango wa skauti na TAKUKURU wamesema watakuwa sehemu ya jamii inayopinga rushwa na kusambaza elimu kwa wengine.

Chama cha skauti kilianzishwa nchini tanzania mwaka 1912 kimeungana taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU katika mpango uliopewa jina la TAKUSKA ili kusambaza elimu sehemu mbalimbali ikiwemo vijijini kwa kushirikisha wanakijiji na wanafunzi…