Kahama FM

Wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS)Manispaa ya Kahama watakiwa kujitathmini.

June 1, 2021, 6:18 pm

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) UMMY MWALIMU

Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) wilayani Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kujitathmini katika utendaji kazi wao, ikiwa ni pamoja na kuzuia ukataji miti na kuchukua mbao kwa wafanyabiasha.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) UMMY MWALIMU, wakati alipotembela eneo la wafanyabiashara na wajasilimali zongomela Dodoma katika manispaa ya Kahama, ambapo amesema kuwa serikali inaendelea kutatua changomoto zinazowakabili wanachi.

Kwa upande wao wafanyabiashra wa eneo hilo la Zongomela Dodoma wamesema kuwa TSF wamekuwa wakivuna misitu katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na mbao na milango kwa madai ya kuwa zinavunwa pasipo na utaratibu.

Naye mbunge wa jimbo la Kahama mjini JUMANNE KISHIMBA ametaka kuundwa kwa kamati ndogo kwa ajili ya kuondoa hali ya kuonewa kwa wafanyabiashara na wajasilimali katika eneo hilo, pamoja na kukagua na kuwakamata wasio fuata taratibu za TFS katika uvunaji wa mbao.

INSERT……MBUNGE KISHIMBA