msalala
Kahama FM

DC KAHAMA:Wauguzi na wakunga zuieni vifo vya wajawazito na watoto.

May 17, 2021, 9:40 am

Serikali imewaagiza wauguzi na wakunga katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuhakikisha wanazuia vifo visivyokuwa  vya lazima vya  akinamama wajawazito na watoto kwa kutoa huduma za afya stahiki  na kwa weledi utakaowezesha wananchi kufurahia upatikanaji wa huduma za matibabu.

Anamringi Macha,Mkuu wa wilaya ya Kahama

Kauli hiyo imetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani,ambapo katika halmashauri hiyo yamefanyika katika kata ya Segese yakiwa na ujumbe usemao wauuguzi ni sauti inayoongoza dira ya huduma ya afya.

Amesema kuwa idadi ya vifo vya akinamama wajawazito mwaka 2020 ilikuwa vilikuwa sita na kwa mwaka huu hakuna kifo hata kimoja, kwa upande wa watoto wachanga mwaka jana vilikuwa 23 na hadi kufikia mei mwaka huu vifo vilivyoripotiwa ni sita.

Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Kahama.

Macha alisema kuwa serikali imejipanga kikamilifu kutatua kero zinaikabili sekta ya afya kwa kuleta wataalamu wa afya na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuhakikisha wajawazito na watoto wanapata huduma bora na kuwaomba wahamishe wananchi wajiunge na bima ya  CHF iliyoboreshwa  

Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Kahama akizungumzia CHF iliyoboreshwa.

Pili Paul ni  Muunguzi mkuu wa halmashauri hiyo  amesema kuwa halmashauri hiyo inauhaba wa wauguzi na wakunga na kuiomba serikali kutoa kipaumbele kwa kuleta watumishi katika zahanati na vituo vya afya vya kijijini ambako bado kunamwamko mdogo wa jamii kuwaruhusu wajawazito kujifungulia hospitalini.

Amesema kuwa Kwa sasa wanawakunga na wauguzi 98 sawa na asilimia 53 wanaoendelea kutekeleza majukumu yao ya kazi kila siku na wanaohitajika ni 185 ambapo kwa sekta ya wauuguzi wanaotakiwa ni 85 sawa na asilimia 47 hivyo ni budi kwa serikali kuongeza watumishi haraka.

Sauti ya Pili Paul ni  Muunguzi mkuu wa halmashauri ya Msalala.