Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
25 November 2026, 12:15 pm

“Mazingira salama ya kazi huongeza tija na furaha kwa wafanyakazi.” Kaimu Mkurugenzi Saidi Ramadhani
Na Jesca Mwita
Zaidi ya Wahudumu taka 40 waliopo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda wamepewa mafunzo ya Usalama na Afya mahali pa kazi yaliyodhaminiwa na Shirika lisililo la Serikali ECO SAFE ORGANIZATION kupitia mradi wa Kuimarisha Usalama na Afya mahali pa kazi
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Said Ramadhani ambapo amelipongeza shirika hilo kwa kuona umuhimu wa elimu ya usalama na afya kwa wahudumu taka na kuamua kuwapatia mafunzo na vifaa vya usalama kazini. Aidha Kaimu Mkurugenzi amewataka Wahudumu taka kutumia vema elimu waliyopata kulinda afya zao na pia kutumia vema vifaa walivyopewa katika shughuli iliyokusudiwa.

