Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
8 August 2025, 8:12 pm

”Chama cha NLD ni chama kikongwe hakuna mtu asiyekifahamu tumeteua Wagombea wa udiwani katika kata zote 13 za Mji wa Bunda” Tosile Habiya katibu chama cha NLD mkoa wa Mara
Na Amos Marwa
Katibu wa chama cha National league for Democracy (NLD) mkoa wa Mara Tosile Habiya amesema chama hicho kimejiandaa vizuri kwelekea uchaguzi mkuu ili kuvuna ushindi zaidi ya chama chochote cha upinzani.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari na kusema kuwa wameteuwa wagombea bora ili kuweza kushinda ubunge katika majimbo yote matatu ya wilaya ya bunda na kata zote za Mji wa Bunda. Ameongeza kuwa Agosti 6, uongozi wa chama hicho ulitoa Ilani kama dira ya mwelekeo wa kisera na kumchagua Doyo Hassan Doyo kuwa mgombea urais , kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo.