Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
12 November 2026, 12:41 pm

Mtu mwenye ulemavu Delti Sagare anajishughulish na ujasiriamali kujiingzia kipato. Picha na mtandao
“Tunapoenda kuomba mkopo tunakutana na vikwazo vingi, tunaambiwa tuwe zaidi ya mtu mmoja hivyo inatuwia vigumu”. Delti Baraka Sagare
Na Jesca Mwita
Watu wenye mahitaji maalumu Halmashauri ya Mji wa Bunda wameiomba serikali kutoa mikopo ya asilimia kumi iliyotengwa na serikali kwa wakati ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na Bunda FM Radio mmoja wa watu wenye ulemavu Delti Baraka amesema kupata mikopo wanapitia changamoto na kuomba waondoe vikwazo ili waweze kupata mikopo hiyo isiyokuwa na riba kwa urahisi.
Aidha watu wenye ulemavu wamesema jamii inapaswa kuacha mtazamo hasi wa kuwanyanyapaa kwani wao ni sehemu ya jamii na nguvu kazi ya taifa katika nyaja ya Uchumi na maendeleo kwa ujumla.