Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
20 November 2026, 9:42 am

Viongozi wanasisitiza kuwa afya duni inakwamisha uzalishaji, na hivyo “ni muhimu kila mwananchi kuona thamani ya kuwa na bima ya afya ili apate huduma kwa wakati anapohitaji”.
Na Jesca Mwita
Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda wametakiwa kujiunga na bima ya afya kwa wote (NHIF) kwa gharama nafuu ili waweze kunguza gharama za matibabu pini wanapopata changamoto za kiafya
Hayo yamesema na Mratibu wa Bima ya Afya kwa wote Said Khalifa akizungumza na Watendaji wa Kata, na Wenyeviti wa mitaa Mjini Bunda wapewa semina kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote amesema zaidi ya huduma ya 372 kutolewa na bima ya afya kwenye vituo vya afya vya serikali
Aidha amewaomba viongozi hao kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kujiunga na bima ya afya kwa wote kwani huduma hii itapunguza kadhia ya kuhangaika kupata matibabu pindi wanapougua na hivyo kuwa na jamii yenye afya bora na nguvu katika kujiletea maendeleo.
