Vwawa FM Radio

DSW yafanya kikao kazi na NGO’s Songwe

25/03/2026, 12:11

Picha ya logo ya DSW Tanzania. Picha na mtandao(DSW website)

Lengo la kikao hicho ni kufahamu NGO ipi inafanya nini na wapi.

Na Devi Mgale

MBOZI

Shirika lisilo la kiserikali la DSW limefanya kikao kazi na mashirika mengine kumi yasiyo ya kiserikali (NGO’s) yanayojihusisha na afua za uwezeshaji wa vijana, afya, kupinga ukatili pamoja na uwezeshaji kiuchumi, Machi 24 katika ofisi za Mamlaka ya Mji Mdogo Vwawa, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Akizungumza katika kikao hicho, mwezeshaji kutoka DSW, Peter Owaga, amesema kuwa lengo la kikao hicho  ni kufahamu NGO ipi inafanya nini na wapi na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa NGO’s wilayani Mbozi, Tumpale Mndekesye, ametoa wito kwa mashirika hayo kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa mamlaka husika ili kurahisisha ufuatiliaji.

Sauti ya Tumpale Mndekesye

Mkurugenzi wa shirika la EFAD, Elisha Shombe, ameshukuru kwa umuhimu wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo  ila wafanye kazi kwa weledi.

Sauti ya Elisha Shombe

Aidha, Kaimu Mratibu kutoka shirika la WISCO la usaidizi wa kisheria Christopher Lusoko amesema kubadilishana uzoefu kunawapa urahisi wa kushirikiana.

Sauti ya Christopher Lusoko