Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
24/02/2026, 20:20

Wanawake katika wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wamechoka kuibiwa viatu wakati wa misiba.
Na Mkaisa Mrisho
Wanawake wa Vwawa wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe wameibuka na kero ya kuibiwa vitu vyao ikiwemo viatu au ndala kwenye misiba hali inayowalazimu kuviweka kwapani wakati wa maombolezo.
Wanawake hao akiwemo Magreth Siwakwi na Prisca Nchinga wameiambia Vwawa FM leo kwamba wezi hao ni wanawake wenzao ambao huiba viatu au ndala mpya na kuziacha ambazo zimechakaa.
Pia wamewataka wanawake ambao wanafanya vitendo hivyo kuwa wastaarabu kwa kufuata kilichowapeleka msibani ili kuepusha kero za aina hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Mpakani kilichopo Vwawa Dismas Silayo amesema vitendo hivyo vipo na kwamba baadhi yao huiba mpaka fedha na simu na kwamba amekuwa akikemea vitendo hivyo ambavyo vimeanza kupungua.