Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
November 27, 2025, 6:58 am

Mbolea ya ruzuku inauzwa kwa bei tofauti na bei elekezi ya serikali
Na Stephano Simbeye
Meneja wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Joshua Ng’ondya amesema mbolea hiyo imekutwa ikiuzwa katika duka la wakala aitwaye Hemed Gira ambapo amesema baada ya kupata taarifa ya ulanguzi huo waliweka mtego na kumnasa akiuza mbolea hiyo kwa bei ya Sh. 95,000 badala ya bei ya ruzuku ya Sh. 76000.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir Omari Makame amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali na kutokubali kulanguliwa kwani bei za mbolea ya ruzuku ni Sh.76000 kwa mfuko wa kilo 50.
Mmoja wa mkulima aliyekutwa na mbolea aliyouziwa kwa bei ya Sh.90000 Osia Mwaigaga amesema alikuwa ameanza kupanda mahindi pasipo kutumia mbolea, lakini alipopata taarifa ya kuwepo mbolea kwa wakala huyo aliamua kwenda kuinunua bila kujali bei.
Naye afisa mauzo wa wakala wa Shikombola Agrovet iliyopo Mlowo Hamadi Kasanga amesema tayari amepokea maroli 22 yenye uwezo wa kubeba tani 30 kila moja na mengine 15 yapo njiani yanakuja.