Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
October 16, 2025, 8:02 am

Kwa ajili ya watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda (njiti)
Na Ezekiel Mwinuka
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Crispin Chalamila amekabidhi vifaa hivyo leo na kwamba vimenunuliwa kwa michango ya watumishi nchini wa Takukuru nchini kwa lengo la kuunga juhudi za Serikali kwenye uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Mkurugenzi wa idara ya watoto kutoka hospitali ya Rufaa mkoa wa Songwe Dkt Antia Kakwala amesema hospitali hiyo mpaka sasa imepokea watoto njiti 240 na kwamba mashine hizo zinaenda kuwasaidia kwenye utoaji wa huduma.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt.Juma Ramadhani Juma amesema hospitali hiyo kwa sasa inatoa huduma zote ambazo zinatolewa na hospitali za rufaa hapa nchini.
Pia Mganga mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt.Boniface Kasululu amesema licha ya mkoa wa Songwe kupiga hatua katika kupunguza vifo vya watoto wachanga lakini bado hali hairidhishi.