Vwawa FM Radio

Mjadala mkali waibuka Songwe kuhusu maana ya ilani za vyama

August 22, 2025, 12:42 pm

Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Songwe wakishiriki mdahalo kuhusu maana ya ilani za vyama vya siasa. Picha: Mkaisa Mrisho

Baadhi ya wakazi wa Songwe wameeleza uelewa wao kuhusu ilani za vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu, huku wanasiasa waandamizi wakifafanua maana halisi ya ilani.

Na Mkaisa Mrisho

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Songwe wamezungumzia uelewa wao kuhusu kitu kinachoitwa ilani kwenye vyama vya siasa.

Vyama vya siasa karibu vyote vitaanza kunadi ilani zao kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 28, kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani.

Wakihojiwa kuhusu uelewa wao, baadhi ya wakazi wa wilaya ya Mbozi wameeleza mitazamo tofauti kuhusu maana ya ilani.

Sauti ya baadhi ya wakazi wa mkoa wa Songwe wamezungumzia uelewa wao kuhusu Ilani.

Wengine ambao wametoa maoni yao ni  Osward Mwambene na Timoth Lwila ambao wamesema ilani ni ushawishi unaotolewa na wagombea kupitia vyama vyao ili waweze kupata nafasi ya kuongoza wananchi.

Sauti ya Osward Mwambene na Timoth Lwila wakieleza maana ya Ilani

Hata hivyo, wanasiasa wawili waandamizi akiwemo Kaimu Katibu wa Chama cha NCCR–Mageuzi mkoa wa Songwe, Edson Kanemile, na Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Songwe, Eliniko Mkola, wamefafanua kwa kina maana halisi ya ilani.

Sauti za Kaimu Katibu wa Chama cha NCCR–Mageuzi mkoa wa Songwe, Edson Kanemile, na Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Songwe, Eliniko Mkola wakifafanua kuhusu Ilani