Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
May 14, 2025, 11:30 am

Ni chakula cha asili, wanadai wanakipenda kuliko nyama ya ng’ombe au mayai
Na Mwandishi Wetu
Baadhi ya Wakazi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wametoa wito wa kuenzi vyakula vya asili kikiwamo kikanda maarufu kwa jina la kinaka. Wakizungumzia kuhusu Kinaka au kikanda ambacho wakazi wa Mbozi wanakipenda kuliko nyama watu ambao wamejitambulisha kwa majina ya Lyidia , Fikiri, Deshesela wanaeleza wanavyokifahamu kinaka
Aidha naye Seven Mwashiuya wa Kitongoji cha Isangu Mbozi amefafanua zaidi kuhusu Kinaka na ulaji wake kwa watoto.
Hata hivyo chakula hicho kina utaalamu wake wa kukitengeneza. Mmoja wa wapikaji wa kikanda au kinaki anaeleza
Aidha mpikaji mwingine anasema kiazi pori ambacho ndicho kinaki chenyewe upatikanaji wake ni mgumu. Kwa hali hiyo wengi wanafuata vinaka nchi za Malawi na Zambia