Uyui FM
Uyui FM
27 September 2025, 7:50 pm
Na Wilson Makalla
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amekabidhi magari matatu kwa Halmashauri za Manispaa ya Tabora, lgunga na Sikonge, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa viongozi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Chacha, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa magari hayo ambayo yatakuwa msaada katika kuongeza ufanisi na uwezo wa viongozi katika kusimamia majukumu ya kila siku.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amesema magari hayo yatakuwa chachu ya utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi, ikiwemo migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa Mkoani humo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Thomas Mnyinga na mkuu wa wilaya ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Upendo Wella wameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa vifaa muhimu kwa ajili ya kuimarisha huduma kwa wananchi, huku wakiahidi kuyatumia magari hayo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili kuleta tija na ufanisi wa kazi.
